Proverbs 1:10-15


10 aMwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,
usikubaliane nao.

11 bKama wakisema, “Twende tufuatane;
tukamvizie mtu na kumwaga damu,
njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;

12 ctuwameze wakiwa hai kama kaburi,
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.

wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.

13 Tutapata aina zote za vitu vya thamani
na kujaza nyumba zetu kwa nyara.

14 eNjoo ushirikiane nasi,
vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”

15 fMwanangu, usiandamane nao.
Usiweke mguu wako katika njia zao,
Copyright information for SwhKC